Comments Off on Muigizaji aanguka na kufariki ‘akishuti’ filamu
Muigizaji wa kiume wa Afrika Kusini kutoka eneo la Centurion, Gauteng amefariki dunia baada ya kuteleza na kuanguka kwenye maporomoko ya maji wakati wa utayarishaji wa filamu, Drakenspberg.
Jeshi la Polisi la eneo la KwaZulu-Natal kupitia msemaji wake, Thulani Zwane limesema kuwa tukio hilo limetokea Alhamisi wiki hii majira ya saa 11 na dakika 15 jioni.
“Walikuwa bize wakiandaa filamu, alitereza na kuanguka kwenye maporomoko ya maji. Timu yetu ya uokoaji haikufanikiwa kufika jana (Jumatano) kwa sababu eneo hilo lilikuwa hatari sana,” alisema Zwane.
Aidha, Ijumaa timu hiyo ya uokoaji ilifika katika eneo hilo na kufanikiwa kuupata mwili wa muigizaji huyo ambaye jina lake halikuwekwa wazi akitajwa kuwa na umri wa miaka 39.
Mwili huo ulipatikana majira ya saa nne asubuhi ukiwa katikati ya miamba ya maporomoko ya maji.