Beki kisiki wa Simba kwa sasa Yusuph Mlipili, ambaye ameanza kupata nafasi ya kucheza na kudumu katika kikosi cha kwanza tangu alivyoondoka kocha Mkameruni, Joseph Omog alisema mechi ya kuonesha ana uwezo ni hiyo ya watani.
HOMA la pambano la watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga ambalo litapigwa Aprili 29, limeanza kufukuta kwa kila timu kuanza mikakati ya mechi hiyo ingawa wakiwa na mechi nyingine mbele yao kabla ya kukutana kwao.
Beki kisiki wa Simba kwa sasa Yusuph Mlipili, ambaye ameanza kupata nafasi ya kucheza na kudumu katika kikosi cha kwanza tangu alivyoondoka kocha Mkameruni, Joseph Omog alisema mechi ya kuonesha ana uwezo ni hiyo ya watani.
Alisema mechi ya Simba na Yanga ni rahisi mchezaji kucheza vizuri na kuonekana hata kuitwa katika timu ya Taifa, thamani yako inaongezeka ndani ya timu au hata nje, lakini ni rahisi kuonekana huna maana kama utashindwa kucheza vizuri.
“Nafanya mazoezi mengi na ya kutosha bila kusahau kumuomba Mungu ili kuniongoza kunipa afya njema ili niweze kucheza vizuri zaidi ya hapa mechi zilizokuwa mbele yangu ili makocha kunipa nafasi ya kucheza mechi na Yanga na nyingine zaidi,” alisema.
“Kama nitapata nafasi ya kucheza mechi hiyo nitajituma kadri ambavyo naweza ili kucheza vizuri.”