HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 9 Aprili 2018

Nikki Mbishi amcharua Steve Nyerere, awataka Bongo Movie waache kudai haki zao

Rapa Nikki Mbishi amewataka Waigizaji wa filamu nchini Tanzania ‘Bongo Movie’ waache kuhangaika kudai haki zao kwa sasa, na badala yake wajipange kwanza kutengeneza kazi nzuri ambazo zitawavutia watazamaji ndio waanze michakato ya kudai haki zao za msingi

Akizungumza na Bongo5, Nikki Mbishi amesema anashangaa kuona Bongo Movie wanahangaika kupoteza nguvu nyingi kudai haki wakati kazi zao mbovu.

Kwa upande mwingine, Nikki Mbishi amemuwasha muigizaji wa filamu na mchekeshaji, Steve Nyerere kwa kitendo chake cha kuzikosoa tuzo za filamu za SZIFF zilizofanyika wiki iliyopita kwa madai kuwa tuzo hizo kuna watu walipata ambao hawakustahili.

Nikki amesema amesononeshwa na kauli za Steve Nyerere kwani kitendo cha Azam TV kuanzisha tuzo hizo ni chachu ya kukuza tasnia ya filamu ambayo kwa sasa inaonekana kuchechemea.