Rais John Magufuli amewataka viongozi wa madhehebu ya dini kuhubiri na kusisitiza amani ambayo ni msingi wa maendeleo
Amesema hayo leo Aprili 8 katika misa ya kusimikwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Isaac Amani iliyofanyika katika parokia ya mtakatifu Theresia mjini humo Amenukuu maandiko matakatifu kutoka kwenye vitabu mbalimbali vya biblia yanayosisitiza amani.
Kuhusu maombi matatu yaliyotolewa na Padri Aloyce juu ya kuhamishwa Shule ya Msingi Naura ambayo ilianzishwa mwaka 1950 ikiitwa St Theresa School mali ya Kanisa hilo ambayo ilitaifishwa na Serikali mwaka 1967 alisema suala hilo lina changamoto kulipatia majibu ya haraka.
"Nikitoa tamko la kurejesha shule hii leo litasumbua sana kila mali zilizotaifishwa mwaka 1967 zitatakiwa kurejeshwa nami sitaki mgogoro huu,"
alisema Rais Magufuli Alisema anaamini kila jambo lina wakati wake na waendelee kumuombea ili apate amani ya kutoa uamuzi sahihi