HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 11 Aprili 2018

Serikali ya Tanzania imezindua kampeni ya chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi.

Serikali ya Tanzania imezindua kampeni ya chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi.

Zaidi ya wasichana laki 6 walio na umri kati ya miaka 9 hadi 14 watachanjwa nchini nzima.

Image captionDuniani, kuna zaidi ya wanawake 260,000 wanaofariki kwa sababu ya saratani ya shingo ya kizazi

Huenda chanjo hii ikawakomboa wanawake na wasichana wengi kama wakijitokeza na kupata chanjo mapema zaidi.

"Saratani ya shingo ya kizazi ndio inayojitokeza zaidi Tanzania na ni chanzo cha vifo na magonjwa yanayohusiana na saratani miongoni mwa wanawake nchini."meneja wa mradi Daphrosa Lyimo aliiambia BBC.

Image captionMsichana mmoja akiandikishwa katika zoezi la uzinduzi

"Duniani, kuna zaidi ya wanawake 260,000 wanaofariki kwa sababu ya saratani hii, ambayo inazuilika na inatibiwa ikigunduliwa mapema." aliongezea Bwana Lyimo

Serikali ina matumaini kuwa kampeni hiyo itapunguza gharama za afya. Kumuuguza mgonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kunaweza kugharimu takriban dola za Marekani elfu 2 wakati dola 15 zitatumika kuwachanja wasichana maafisa walisema.

Mambo kumi unayoweza kufanya kupunguza hatari ya kuugua saratani:

Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote

Hakikisha nyumbani kwako hamna moshiKula chakula chenye afyaKunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani

Hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HP

VEpuka kuchomwa sana na miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo.

Punguza uchafuzi wa hewa ndani na nje ya nyumbaJishughulishe kuupa mwili mazoezi

Punguza unywaji wa pombeJitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani.