HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 23 Aprili 2018

Sheria namba tatu ya FIFA inayozungumzia idadi ya wachezaji wa timu uwanjani inafafanua nini kifanyike baada ya refa kubaini mtu kuzidi uwanjani.

Sheria namba tatu ya FIFA inayozungumzia idadi ya wachezaji wa timu uwanjani inafafanua nini kifanyike baada ya refa kubaini mtu kuzidi uwanjani.

Kama refa angelibaini tukio hilo mapema alipaswa kulikataa bao la Mbeya City ikiwa walifunga bao lao wakiwa wako 10 uwanjani.

Na hata kama angelibaini baadae kabla ya mchezo kumalizika, alipaswa kusimamisha mchezo, kumuadhibu mchezaji aliyezidi kisha kutoa taarifa kwa kamisaa wa mchezo juu ya tukio hilo.

Tukio hilo liliripotiwa kwa kamisaa wa mchezo punde tu baada ya mchezo kumalizika hivyo Kamati ya saa 72 itakapokutana huenda ikawa moja ya ajenda yake.

Ukifuatilia video iliyotolewa na Azam TV unaweza kubaini kwa urahisi kuwa ni kweli Mbeya City ilikuwa na wachezaji 11 dimbani pamoja na mlinda lango.