HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 28 Aprili 2018

Simba anatokaje kwa mfano

Moja ya faida kubwa iliyopata Simba msimu huu ni baadhi ya timu walizokutana nazo kuogapa kucheza mpira, pengine ni sababu ya vitisho au nyinginezo.
Simba ina udhaifu mkubwa katika mfumo wao wa ulinzi hasa wanapokuwa hawana mpira. Ndio maana wakati mwingine kocha wao analazimika kuwatumia walinzi wa pembeni kuwa viungo ili kuficha madhaifu hayo.
Aidha aina ya mfumo wanaoutumia wa 3-5-2 unatoa nafasi kwa washambuliaji wajanja kuweza kutumia mianya inayoachwa pembeni kusababisha madhara.
Hakika mchezo wa Jumapili watakuwa na kazi kubwa ya kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga ambao wameapa kuwalaza na viatu.
Yusuph Mhilu, Raphael Daudi, Pius Buswita, Ibrahim jib na Obrey Chirwa hawawezi kuwaacha salama.
Amissi Tambwe amerejea pia lakini huu sio aina ya mchezo unaofaa kuanza kutumika kwa kuwa amekaa nje kwa muda mrefu.
Mchezo huu umewadia wakati ambao Lothi amerejea katika kiwango chake na anaonyesha kipaji chake halisi. Lothi amekuwa kama ingizo jipya kwenye kikosi cha Yanga.
Simba inakutana na Yanga wakati ambao winga Yusuph Mhilu amekomaa. Mhilu hakuwemo kwenye mchezo wa kwanza timu hizo zilipotoka sare ya bao 1-1.
Yanga pia itaimarika zaidi kwenye sehemu ya kiungo hasa baada ya kurejea kwa Thabani Kamusoko ambaye sasa amepona kabisa majeraha yake yaliyomuweka nje kwa zaidi ya miezi mitatu.
Yeye pamoja na Papi Tshishimbi ndio watakaoamua ushindi wa Yanga wakitarajiwa kuongoza sehemu ya kiungo kwa kushirikiana na viungo wa pembeni.
Safu ya ulinzi ya Yanga haina hofu tena baada ya kupona kwa Andrew Vicent na Kelvin Yondani. 
Pia yupo Abdallah Shaibu 'Ninja' ambaye bila wasiwasi wowote anaweza kuwadhibiti washambuliaji wawili wa Simba, Okwi na Bocco. 
Walinzi wa pembeni ndio usiguse kabisa. Ushindani uliopo baina yao umeweza kuimarisha viwango vyao kwa kiasi kikubwa.
Juma Abdul, Hassani Kessy, Haji Mwinyi na Gadiel Michael yeyote anaweza kucheza mchezo huo bila ya wasiwasi wowote.
Wachezaji wa Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakifahamu kuwa bila ya ushindi hakuna ubingwa msimu huu. 
APRIL 29 NI SIKU YA KUWASHIKISHA ADABU

PATA HABARI HARAKA ZAID KWENYE SIMU YAKO
 INSTALL KATISHA BLOG APP

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO

    BONYEZA HAPA KWENYA K
INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD KATISHA BLOG APP IN GOOGLE PLAY STORE ...ANDIKA KATISHA ...SEARCH