HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 19 Aprili 2018

Yanga Kunasa Mabilioni

Kwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika Yanga tayari imejihakikishia kupata zaidi ya Mil 625 bila ya kujali itamaliza nafasi ya tatu au ya nne kwenye kundi lake.

Kila kundi litakuwa na timu nne hivyo hata ikimaliza nafasi ya mwisho itapokea kiasi hicho cha pesa.

Lakini ikimaliza nafasi ya pili au ya kwanza katika kundi lake itafanikiwa kutinga hatua ya robo fainali na dau litaongezeka kuwa karibu Mil 800.

Ikitinga nusu fainali dau litazidi kupanda na kufika Bil 1 wakati ikitinga fainali na ikapoteza mchezo wa fainali italamba Bil 1.4.

Ikitwaa ubingwa italamba zaidi ya bil 2.8!

Sasa hapa ndipo umuhimu kuzichanga vyema karata katika michuano hii unaonekana kuliko hata ligi kuu ya Vodacom kwani bingwa wake analipwa Mil 80 tu!

Hata hivyo kutwaa ubingwa wa VPL bado ni muhimu ili kujihakikishia kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao hasa ikizingatiwa tayari Yanga imeondolewa kwenye michuano ya kombe la FA

Lakini ukweli ni kwamba msimu huu Yanga ndio klabu itakayokuwa imeingiza pesa nyingi kuliko timu yoyote hata kama itashindwa kutetea ubingwa wake.