HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 30 Aprili 2018

Yanga yatoa msimamo wake juu ya Chirwa


Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligii Kuu Tanzania Bara na wawakilishi pekee kutoka nchini Tanzania katika mashindano ya kimataifa Yanga, imekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii na kusema sio kweli kuwa nyota wao Obrey Chirwa hatoweza kucheza mechi ya leo kutokana na kadi 3.
Msimamo huo umetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Dismas Ten kupitia ukurasa maalum wa klabu yao yakiwa yamebakia masaa machache kabla ya mtanange huo wa kukata na shoka kuanza kulindima katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.
"Sio kweli kwamba Obrey Chirwa ana kadi tatu za manjano kama watu wanavyozungumza kwenye mitandao ya kijamii na sehemu zinginezo", amesema Dismas.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katikia mechi ya 'watani wa jadi' itakayo ng'urumishwa majira ya saa 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.
Msikilize hapa chini Dismas Ten akifunguka zaidi juu ya Obrey Chirwa.

BONYEZA HAPA CHINI ILI UWEZE

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD KATISHA BLOG APP IN GOOGLE PLAY STORE ...ANDIKA KATISHA ...SEARCH


PATA HABARI KWA UHAKIKA ZAIDI NA KATISHA BLOG