HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 9 Mei 2018

African Lyon yamleta kocha mfaransa

Mmiliki wa Klabu ya soka ya African Lyon iliyorejea ligi kuu msimu huu, Rahim Kangezi maarufu ‘Zamunda’ amesema wameleta kocha kutoka nchini Ufaransa mwenye leseni A ya Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA).
Zamunda amesema ujio wa kocha huyo ambaye hajaweka wazi jina lake mpaka taratibu za mkataba wao zitakapo kamilika ni sehemu ya uwezeshaji wa wafadhili wao ambao wanataka kuona timu hiyo ikifanya vizuri kwenye michuano ya ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.
“Tunataka kufanya vizuri msimu ujao, tuwe timu ya ushindani tuonyeshe tofauti na tufanye vizuri tofauti na misimu na ili hayo yafanikiwe, lazima tuwe na maandalizi mazuri ikiwemo kuleta kocha kama huyu mwenye uwezo,”alisema.
African Lyon ilipanda ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu wa 2009/2010 ikiwa chini ya umiliki wa mfanyabiashara Mohamed Dewji 'Mo' kabla ya msimu wa 2015/16 kushuka daraja lakini msimu huu imerejea na kuanzia msimu ujao itaanza kuonekana.
Mbali na African Lyon timu nyingine zilizopanda daraja ni KMC ya Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Biashara United ya Mara na Alliance Schools ya Mwanza. Moja ya wachezaji waliokuwa na Lyon wakati inashuka daraja ni mlinda mlango namba moja wa Yanga Youthe Rostand
Apks >> News & Magazines >> Katisha Blog

Katisha Blog apk

This apk is safe to download