HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 22 Mei 2018

Baada ya kumkosa Salamba, Yanga yahamia kwa straika wa Ndanda - Sports Kitaa


Klabu ya Yanga SC imeanza kumuwania mshambuliaji wa Ndanda SC, Tiber George kwa ajili ya kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji.

Licha ya taarifa hizo kueleza kwamba tayari Yanga imekwishafika mezani kwa ajili ya majadiliano na Ndanda, msemaji wake Dismas Ten amekataa kuthibitisha ukweli wake huku akisisitiza kuwa kamati ya usajili ndiyo inayohusika na masuala ya usajili.

Ten amesema Tiber ni mchezaji mzuri na anastahili kuichezea Yanga na kudokeza kuwa kipindi cha usajili kitakapofika, kamati yao ya usajili itaweka hadharani kila kitu.

“Ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa, na kama akiendelea hivyo atafika mbali … kuhusu kuja Yanga, kamati ya usajili ndiyo inahusika lakini anaweza kucheza timu yoyote kwa sababu mpira ni kazi yake,” amesema Ten.

Kwa upande wake mchezaji mwenyewe amesema yuko tayari kujiunga na timu yoyote inayomuhitaji ikiwemo Yanga endapo itafikia makubaliano na uongozi wa Ndanda.

Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni siku chache baada ya ombi la Yanga kumuomba mshambuliaji wa Lipuli FC Adam Salamba, kugonga mwamba kwa kile kilichoelezwa na Lipuli kuwa kanuni haziruhusu.