HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 22 Mei 2018

Ni yanga vs mbao leo

Kikosi cha Yanga leo kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kucheza na Mbao FC katika moja ya michezo ya kukamilisha ratiba.

Yanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, inazo sababu za kusaka ushindi leo.

Yanga inahitaji kumaliza rekodi mbaya ya kucheza michezo tisa bila ya kushinda ikiwemo michezo sita bila kufunga bao.

Ushindi kwenye michezo yake mitatu iliyobaki, utawawezesha mabingwa hao wa zamani kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Kwa sasa Azam FC iko kwenye nafasi ya pili ikiwa imeizidi Yanga alama saba imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Yanga.

Mbao FC imekuwa ikiipa wakati mgumu Yanga timu hizo zinapokutana. Hata hivyo sio kwenye uwanja wa Taifa.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Taifa Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Lakini michezo mitatu iliyofuatia ambayo yote ilipigwa katika uwanja wa CCM Kirumba Yanga ilifungwa.

Katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliopigwa CCM Kirumba Mbao FC ndio ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga msimu huu kwa kuichapa mabao 2-0 

Wachezaji wa Yanga wataingia kwenye mchezo huo wakiwa wanatambua kuwa wanahitaji kushinda ili kurudisha imani ya mashabiki kwao.