HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 28 Mei 2018

Huyu hapa mchezaji mdogo kuliko wote VPL

Kiungo wa Lipuli ya Iringa, Shaaban Ada, 17, ndiye kinda aliyecheza mechi nyingi zaidi Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wa 2017/18, unaomalizika leo.

Ada ambaye alizaliwa 2001 alianza kuichezea timu ya taifa chini ya miaka 17, Serengeti Boys kabla ya kujiunga na Lipuli ambayo ameichezea mechi 20 za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kiungo huyo, anasema kwenye mazungumzo maalumu na jarida hili la Spoti Mikiki anavutiwa na uchezaji wa Thabani Kamusoko na mara zote amekuwa akijifunza vitu vingi kutoka kwake.

“Jamaa napenda uchezaji wake, anajua kucheza kwa nafasi, huwa natumia muda wangu mwingi kumtazama, Kamusoko kwa lengo la kuchota ujuzi,” anasema kinda huyo.

Ada ambaye kwa sasa anaichezea timu ya taifa chini ya umri wa miaka 23 ‘Ngorongoro Heroes’ anasema Lipuli ndiyo timu yake ya kwanza kuichezea Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Lipuli ilivutiwa na kiwango changu kwenye yale mashindano ya Afcon nchini Gabon, nilivyorudi fasta walinitafuta na kufanya mazungumzo ya kujiunga nao, watu wangu wa karibu walinishauri kwa umri wangu kuwa niende huko ili niwe na muda mwingi wa kucheza.

“Isingekuwa rahisi kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye vikosi vya Simba na Yanga kama ningeamua kujiunga nao, nashukuru sana benchi langu la ufundi la Lipuli kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuonyesha uwezo wangu,” anasema Ada.

Ada anasema msingi wa mpira wake ulianzia Uswahilini kabla ya kujiunga na kituo cha Karume ambacho mara nyingi kilikuwa na program mbalimbali za vijana nyakati za asuhubi hasa mwishoni mwa juma.

“Buruguni kulikuwa na timu inaitwa Barcelona, hiyo ndio niliyoanza nayo nikiwa mdogo kabisa na kabla sijajiunga na Serengeti Boys nilipitia pale JMK Park baada ya Karume,” anasema.

Mwisho kabisa, Ada anasema pamoja na changamoto zilizopo kwenye soka ndoto yake ni kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.