HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 6 Mei 2018

KUHUZUNIKA PAMOJA: RAIS MAGUFULI ASIMAMISHA ZIARA NA KUJUMUIKA MSIBANI.

Rais Magufuli akiwa msibani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, jana alilazimika kusitisha ratiba yake kwa muda, na kujumuika na waombolezaji waliokuwa wakiomboleza kifo cha kijana aitwaye James Gerald.

Akiwa njiani kuelekea kufungua daraja lilopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro, Rais Magufuli aliona wananchi wakiwa wamekusanyika katika msiba wa mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, James Gerlad, na ndipo alipoamua kuungana nao na kutoa salamu zake za pole.

Rais Magufuli akitoka msibani

Mara baada ya kutoa rambirambi, Rais Magufuli amendelea na ziara yake, ambapo tayari amekwisha zindua daraja la mto Kilombero liitwalo Daraja la Magufuli (Magufuli Bridge), ambalo lina urefu wa mita 384, huku gharama zake zikitajwa kuwa ni shilingi Bilioni 61.233.

Daraja la Magufuli (Magufuli Bridge) ni daraja kubwa mkoani Morogoro linalopita katika mto Kilombero na linaunganisha maeneo ya Ifakara na Mahenge, hivyo kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa wakazi wa maeneo hayo.