HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 7 Mei 2018

Magufuli apiga marufuku siasa vyuoni


Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kufanya siasa wanapokuWa chuoni bali watumie muda mwingi kusoma na kufanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Tanzania.

Rais Magufuli amesema hayo leo Mei 07 2018 wakati wa ziara katika chuo cha kilimo (SUA) Mkoani Mororgoro ambapo amesema kuwa serikali inatoa fedha nyingi  sana kuwapa mikopo wanafunzi  wa elimu ya juu na kuongeza kuwa hatasita kuchukua hatua.

“Niwaombe wanachuo mpo hapa kwa ajii ya shule, tekelezeni wajibu wenu, msipoteze muda wenu katika masuala yasiyokuwa na tija, tumewapa mkopo watu 6600 nitasikitika sana kama hii mikopo  kutoka kwa wananchi masikini, mfanye manbo ambayo hayaendani na yale ambayo  mmeletwa kufanya, msivigeuze vyuo maeneo ya kufanya siasa” alisema Magufuli

Rais Dkt. Magufuli alisema kuwa serikali yake haitasita kuchukua hatua ikiwemo kuawafukuza chuo wanafunzi ambao watakuwa kinara wa kusababisha migomo na kuongeza kuwa wengi wao ni wale ambao wanakua na matokeo mabaya ya kitaaluma.

Awali Rais Magufuli alipongeza uongozi wa chuo hicho kwa kufanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya utafiti, kilimo na ufugaji na kuahidi kutoa kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa mabweni chuoni hapo.