
Uongozi wa klabu ya @yangasc umethibitisha kuwa wanatarajia kumalizana na wachezaji wake wote wanaodai pesa zao mara timu hiyo itakapotua nchini wakitokea Algeria kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika.
Taarifa ambayo @sokaonline imepata jioni hii inasemekana uamuzi huo umetolewa baada ya kuambulia kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya USM Alger kunako michuano hiyo sababu ikiwa ni kukosekana kwa wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza ambao hawakusafiri na timu.
Wachezaji ambao hawakusafiri na timu ni Papy Tshishimbi, Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Thaban Kamusoko, Kelvin Yondani, Amisi Tambwe na nahodha Nadir Haroub.
#sokaonlineupdates