Mhando, ambaye anapambana na Chiasso yake kuhakikisha inapanda daraja na kushiriki msimu ujao Ligi Kuu Uswizi ni Mtanzania, ambaye alizaliwa na kukulia Italia.
KIUNGO wa Chiasso, Said Mhando amedai ni mfuasi makini wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji kwa kipindi kirefu.
Mhando, ambaye anapambana na Chiasso yake kuhakikisha inapanda daraja na kushiriki msimu ujao Ligi Kuu Uswizi ni Mtanzania, ambaye alizaliwa na kukulia Italia.
“Jina lake nilianza kulisikia wakati akiwa TP Mazembe, ndugu zangu nilikuwa nawasiliana nao kutoka Tanzania walikuwa wakinieleza ubora wake,” alisema Mhando.
Nyota huyo wa zamani wa Brescia ameichezea Chiasso msimu huu dakika 1,844 ndani ya michezo 24 ya ligi hiyo daraja la kwanza ambayo ni maarufu kama Challenge League.