Mkutano Mkuu wa wanachama wa klabu ya Yanga unatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo, May 06, 2018.
Uongozi wa Yanga umewataka wanachama wa klabu hiyo kulipia ada zao za uanachama mapema ili kueopuka usumbufu siku ya Mkutano.
Ni wanachama ‘hai’ pekee watakaoruhusiwa kuingia kwenye Mkutano huo utakaopitisha ajenda muhimu.
Pamoja na maswala mengine, madhumuni makuu ya Mkutano huo ni kupitia na kuidhinisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya Yanga yaliyowasilishwa na Kamati ya utendaji.
Pia kupitia na kuidhisha mapendekezo ya mfumo ya uendeshaji wa klabu ya Yanga yaliyowasilishwa na Kamati ya Utendaji.
Hii ni nafasi adimu kwa WanaYanga kuamua mustakabali wa klabu yao.