KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, Hemed Morocco, amesema yupo tayari kuinoa timu yoyote ikiwamo Yanga iliyotajwa kumpigia hesabu kubeba mikoba ya George Lwandamina aliyerejea katika kikosi chake cha Zesco ya nchini kwao, Zambia.
Yanga kwa sasa wananolewa na Mzambia Noel Mwandila akisaidiana na Shadrack Nsajigwa, ikiwa ni baada ya kuondoka kwa Lwandamina.
Akizungumza na BINGWA jana, Morocco alisema hakuna timu ambayo imefanya naye mazungumzo, lakini endapo itatokea, ikimtengea dau nono yupo tayari kujiunga nayo.
Alisema pamoja na kusikia tetesi za kufuatwa na Yanga, hajaonana na kiongozi yeyote wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akisisitiza: “Endapo watanitaka (Yanga), nipo tayari, kikubwa ninachoangalia ni masilahi.”