HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 12 Mei 2018

Msichana abakwa na kuchomwa moto akiwa hai



Msichana mmoja nchini India amebakwa na kuchomwa moto hadi kufariki na watu hao waliombaka huko nchini India.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 16 alimwagiwa mafuta na kuchomwa moto akiwa nyumbani kwao katika wilaya ya Sagar, na kufanya tukio hilo kuwa la tatu kutokea ndani ya wiki moja.

Polisi wa eneo hilo wamesema msichana huyo aliuawa baada ya kuwaambia watu waliombaka kuwa ataenda kusema kwa familia yake juu ya walichomfanyia.

Matukio kama hayo nchini India yamekuwa yakitokea mara kwa mara, ambapo ndani ya wiki hii limekuwa la tatu, baada ya msichana wa miaka 17 kuchomwa moto hadi kufa na mtu aliyetaka kumuoa, kutokana na kukataa kuolewa naye.