HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 8 Mei 2018

Ninja kakubali yaishe aisee


Tofauti na Tanzania ambako huwa na kiwango cha juu cha joto nyakati za mchana kinachoweza kufika hadi nyuzi 33, Ninja amekutana na mazingira tofauti Algeria ambako nyakati za mchana kiwango cha joto huwa ni nyuzi 17 wakati nyakati za usiku joto hufikia hadi nyuzi 10 za sentigredi.

BEKI Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ni miongoni mwa wachezaji wachache wa Yanga waliofika Algeria kwa mara ya kwanza safari hii ambapo imekuja kucheza dhidi ya USM Algiers akiwa sambamba na Yussuf Mhilu na Pius Buswita, lakini raha za beki kuingia hapa kwa mara ya kwanza zimeingia shubiri kutokana hali ya hewa ya baridi ambayo amekutana nayo huku.

Tofauti na Tanzania ambako huwa na kiwango cha juu cha joto nyakati za mchana kinachoweza kufika hadi nyuzi 33, Ninja amekutana na mazingira tofauti Algeria ambako nyakati za mchana kiwango cha joto huwa ni nyuzi 17 wakati nyakati za usiku joto hufikia hadi nyuzi 10 za sentigredi.

Beki huyo aliliambia gazeti hili kwamba hali hiyo ya hewa inampa shida kwani hakuwahi kukutana nayo kabla ingawa amejitahidi kukabiliana nayo kwa muda wote ambao Yanga ilikuwa Algeria.

“Kiukweli hili baridi la huku ni kali sana na sijawahi kukutana na hali kama hii ambayo imesababisha hadi mafua yaanze kuninyemelea lakini namshukuru Mungu haijaniletea madhara yoyote hadi sasa.

Unajua unapokuwa mchezaji, kuna aina fulani ya mazoezi ambayo unafanya, yanaupa mwili uwezo wa kustahimili mazingira na hali ya hewa tofauti jambo ambalo naamini limenisaidia kuweza kumudu mazingira ya huku ingawa naamini ingekuwa kwa mtu mwingine ambaye hafanyi mazoei, hali ingekuwa tete,” alisema Ninja.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, wakati baridi hilo likionekana kumsumbua Ninja, wenyeji wa hapa wanadai kwamba hiki ndicho kipindi cha kiangazi ambacho ni kizuri kwa wageni kuishi hapa kwani kuna nyakati baridi hufiki hadi nyuzi 5 za sentigredi ambalo hupelekea hadi theluji kuanguka ikitoka angani.