HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 8 Mei 2018

Nuh Mziwanda Awaka Kisa Kubemendewa Mtoto wake "Mimi Sitaki Basi Anipe Mtoto Wangu''

Msanii Nuh Mziwanda amelalamikia kitendo cha mama mtoto wake ambaye alikuwa mke wake, Nawal, kuwa na mahusiano na wanaume wengine tofauti tofauti huku akiwa analea mtoto mdogo aliyeza naye,

Akizungumza na www.eatv.tv, Nuh Mziwanda amesema kinachomuumiza zaidi ni maiasha ambayo mtoto wake anaisha ambayo anahisi si salama, huku mama mtu akimkatalia kumpa mtoto.

“Bora angekuwa amekaa analea mtoto, kibaya zaidi anadate na watu tofauti tofauti wakati bado analea mtoto, mimi sijamkataza kufanya mambo yake, ubaya anadate na watu wengine ambao mimi sitaki, basi anipe mtoto wangu nikae naye, akihitaji kumuona aje amchukue siku mbili tatu amrudishe aendelee na mambo yake, na mwanangu haishi kwenye mazingira mazuri anaishi kwenye mazingira mabaya”, amesema Nuh.

Sakata la Nuh na mke wake Nawal sio mara ya kwanza kufika kwnye vyombo vya habari, lakini Nuh bado anaendelea kulalamika kuwa anayimwa mtoto, licha ya maisha ya mama yake ya kutotulia pamoja.