KAMANDA wa polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Muliro, ametoa ufafanuzi wa Jeshi la Polisi kuhusu Mwalimu wa Shule ya Msingi ya St Florence iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, Ayoub anayedaiwa kuwadharirisha kingono wanafunzi wake wa kike wanne.
Kamanda Muliro amesema jeshi la polisi limeanza kufanya uchunguzi juu ya suala hilo kwa kushirikiana na wanafunzi hao wanne wanaodaiwa kuingiliwa na ‘Ticha Ayoub’ na uchunguzi utakapokamilika watamfikisha mtuhumiwa mahakamani.
Aidha, Kamanda Muliro amesema jeshi la polisi pia linaendelea kumtafuta mtuhumiwa anayedaiwa kukimbia baada ya taarifa za tukio hili kusambaa.
Mapema leo, Wabunge waliihoji Serikali kuhusu hatua gani imechukua baada ya kuwepo kwa taarifa za mwalimu huyo kufanya kitendo hicho kichafu ikwa watoto ambapo Waziri Jenister Mhagama alisema Serikali inalifanyia kazi na itaeleza Bungeni hatua gani imechukua baada ya uchunguzi kukamilika.