Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kutua nchini Algeria saa saba mchana tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger unaotarajiwa kupigwa keshokutwa Jumapili, May 06 2018.
Kikosi cha Yanga kiliondoka jana jioni kikiwa na wachezaji 18 wengi wakiwa vijana.
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema timu hiyo haikwenda Algeria kutalii, bali imekwenda kupambana.
Saleh anaamini wachezaji walio kikosini wataweza kuipa Yanga matokeo ugenini nchini Algeria.
Wachezaji wakongwe ambao hawakusafiri na timu kutokana na sababu mbalimbali ni pamoja na Benno Kakolanya, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Papi Tshishimbi, Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa.