HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 6 Mei 2018

Yanga hii itawaduwaza USM Alger

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu watawakosa nyota wake sita, wakiwa ni mabeki Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Canavaro’, viungo Papy Tshishimbi na Thaban Kamusoko na washambuliaji, Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa.

Mwanza.Wakati Yanga ikitarajia kujitupa uwanjani leo kuwavaa USM Alger  katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho Afrika bila nyota wake wa kikosi cha kwanza.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu watawakosa nyota wake sita, wakiwa ni mabeki Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Canavaro’, viungo Papy Tshishimbi na Thaban Kamusoko na washambuliaji, Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya mashabiki jijini Mwanza walisema kuwa Yanga ina kikosi kipana, hivyo kutokuwapo kwa nyota hao haitazuia kupata matokeo mazuri.

Mhando Madega alisema hadi sasa Yanga kuwa nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu kazi kubwa imefanywa na vijana wadogo walioambatana na timu kuliko waliobaki Dar es Salaam.

“Yanga ina kikosi kipana, kila mmoja ana umuhimu wake ndani ya timu kwa hiyo kutokuondoka kwa hao wachezaji sioni kama itaathiri chochote,” alisema Madega.

Emanuel Majula ‘Ema Yanga’ alisema wanaamini vijana waliosafiri watafanya kazi nzuri na kwamba Yanga haitegemei mchezaji mmoja.

“Ile ni timu kubwa ilisajili wachezaji wa kutosha ambao kila mmoja alikuja kufanya kazi, kwahiyo usifikiri tunategemea mtu mmoja, tuna imani na walioondoka kurudi na matokeo mazuri,” alisema Majula.

Naye Khamis Maluli aliungana na mashabiki hao kuwa lazima chama lao lifanye kweli licha ya kutokuwapo kwa mastaa wao wa kikosi cha kwanza.