HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 4 Mei 2018

Yanga ni wao tu, CAF yaipa ujanja

CAF ambayo ndio wenye mashindano hayo, imeipa Yanga upenyo wa kusajili wachezaji hadi saba endapo tu haikufikisha idadi ya wachezaji 30 kwenye orodha yake ya kwanza iliyowasilishwa mapema mwaka huu.

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeipa Yanga ujanja wa kufanya vizuri kwenye mechi za hatua ya makundi na sasa kila kitu kimebaki kwa timu hiyo kuamua hatma yake.

CAF ambayo ndio wenye mashindano hayo, imeipa Yanga upenyo wa kusajili wachezaji hadi saba endapo tu haikufikisha idadi ya wachezaji 30 kwenye orodha yake ya kwanza iliyowasilishwa mapema mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 5 kipengele kidogo cha 8 cha Kombe la Shirikisho Afrika, timu zote zilizofuzu hatua ya makundi zinaruhusiwa kuongeza wachezaji hadi saba wiki mbili kabla ya kuanza kwa mechi zao.

“Endapo timu haikufikisha wachezaji 30 kwenye orodha ya awali, inaweza kusajili wapya wasiozidi saba wiki mbili kabla ya kuanza kwa mechi zao za hatua ya makundi.

Muda wa usajili utakuwa wazi hadi Agosti 5,” inasema kanuni hiyo.

Hata hivyo, kanuni hiyo imekuwa na changamoto yake kutokana na kipengele kidogo cha 3 (c) kutaka mchezaji anayesajiliwa awe na uwezo wa kushiriki mashindano ya ndani ambayo timu inashiriki, jambo ambalo kwa sasa haliwezakani kwani usajili wa timu za Ligi Kuu umefungwa.

“Mchezaji anayeweza kushiriki michuano ya CAF ni lazima awe na leseni ya timu yake kutoka kwenye shirikisho la ndani, kuwa na leseni ya CAF na awe na uwezo wa kushiriki mashindano ya ndani na ya CAF,” inasema kanuni hiyo.

Baadhi ya maeneo ambayo Yanga imeonekana kuhitaji nguvu kazi mpya ni kiungo na ushambuliaji, lakini changamoto kubwa ni upatikanaji wa wachezaji huru kwa sasa.

Michuano hiyo ya CAF kwa shirikisho na Ligi ya Mabingwa imepangwa kumalizika baadaye Desemba mwaka huu.