HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 31 Mei 2018

Yondani, Yanga mambo fresh tu

Dar es Salaam. Beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani aliyekuwa anatajwa kujiunga na Azam Fc, leo amekutana na viongozi wa klabu yake katika makao makuu ya klabu hiyo (Jangwani) na kumalizana madai ya nyuma katika fedha zake Sh 18 milioni za usajili.

Uongozi wa Yanga umehakikisha wanahangaika kumbakisha mchezaji huyo, lakini kwa sharti la kulipa deni la fedha zake za usajili wa awali.

Baada ya kumaliza kulipa deni hilo, inatajwa beki huyo anakaa tena chini na viongozi wake katika kujua hatma ya mkataba mpya wa kukitumikia kikosi hicho msimu ujao.

Uongozi wa klabu hiyo ukingozwa na Mwenyekiti wa Usajili, Hussein Nyika wamepambana kumbakisha Yondani baada ya kusikia mchezaji huyo anatakiwa na Azam, wanaotajwa kutenga fungu kubwa kwaajili ya usajili msimu huu.