HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 8 Juni 2018

Wabunge warushiana vijembe mtandaoni

Siku moja baaada ya pacha walioungana, Maria na Consolata kuzikwa, kumetokea mzozo baina ya Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela katika akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter.


Mzozo ulianza juzi Juni 6, 2018 baada ya Msigwa kuandika twiti akisema: “DC Kasesela anafanya siasa kwenye msiba wa Maria na Consolata. Bila aibu hajaacha kutaja jina langu akidhani kwa kufanya hivyo itamsaidia kisiasa. Kasesela usitumie huo msiba kwa faida ya kisiasa. Shame on you! Umeshindwa hata kumtambua Meya wa mji.”


Asubuhi ya leo Juni 7, 2018 Msigwa ameandika tena twiti akisema: “DC Kasesela kila wakati is looking for attention! niliwahi kusimuliwa watu wa aina hii! Kukiwa na harusi anatamani awe bwana harusi! Kukiwa na ubatizo anatamani awe mbatizwaji! Kukiwa na msiba anatamani awe jeneza. Boys are always looking for attention, men always have attention.”


Akijibu hilo, Kasesela akaandika: “Mheshimiwa Mbunge is this Real you?! Nimesema neno gani baya?”


Msigwa akaandika: “Umesema mbele ya hadhara kuwa mimi sijatuma rambirambi ulijuaje? Kwani mimi nilipaswa kukupa wewe ? Hao wabunge wa CCM hawajakuambia kama nilichangia! Kwani unadhani watu wa Iringa hawamjui mbunge wao?”


Kasesela: “Omba re play you should not stress yourself nimegundua hukunisikia umeambiwa.”


Msigwa: “Nimekusikia watu walikushangaa sana unaposema eti Rita ni mbunge wa Iringa! Na walikupinga! Umeshindwa kumheshimu Meya wa Mji! Hata wewe hustahili heshima.”


Kasesela: “Sasa Rita Kabati ni mbunge wa wapi.”


Msigwa: “Acha ushamba”


Kasesela: “Mimi nimekubali ushamba toka jana Kaka”


Msigwa; “Kwa Kweli washamba wanaviherehere!”