HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 9 Juni 2018

Wanasiana wakila uroda

-Kulikuwa na kisanga mjini Kitale Ijumaa wakati mwanamume kutoka Kaunti ya Turkana alipatikana peupe akiwa amekwama ndani ya mwanamke baada kushiriki ngono nje ya ndoa


-Kisa hicho kilifanyika baada ya mkewe mwanamume huyo kumwekea mtego aliopewa na mganga


-Mwanamume huyo ambaye ni mteja mkubwa wa lojing’i hiyo akiwa Kitale kununua bidhaa za duka yake alikuwa amesafiri kutoka Lodwar kufanya mapenzi na mwanamke ambaye ni mwenye nyumba ambayo huishi


Kisa hicho kilipelekea msongamano wa magari katika barabara yenye shughuli nyingi ya Laini Moja ambako kuna lojing’i hiyo.

Mwanamume huyo akipelekwa kituo cha polisi na mpenziwe. Picha/Philip Bwayo/TUKO

Mkewe mwanamume huyo alisema alishuku kuwa mwanamume huyo alikuwa akidanganya katika ndoa na mmiliki wa nyumba wanamoishi lakini alikuwa akikana akiulizwa.

“Niliamua kutafuta huduma za mganga anayeishi Kitale baada ya kujua huduma hizo mtandaoni. Alikubali kumwekea mtego na sasa amepatikana,” alisema mwanamke huyo.


Mganga hutengeneza dawa inayowafanya wadanganyifu kukwamana.

Wawili hao waliwekwa ndani ya gari aina ya Toyota Probox na kukimbizwa katika Kituo cha Polisi cha Kitale ambapo baadaye walipelekwa kwa mganga huyo nje ya mji kutenganishwa.


Mganga huyo almaarufu daktari Nduta alifanya matambiko na kuwatenganisha, ambapo mwanamume huyo aliahidi kutorudia kosa hilo, na kuomba mkewe msamaha.



Wakiwa ndani ya gari la polisi. Picha/Phillip Bwayo/TUKO

“Aki mama Brian unisamehe sitawai rudia tena. Nitakuwa mwaminifu kwako kuanzia leo,” alisema mwanamume huyo.


"Mtu akija kwetu akilalamika, huandika majina yao kwa karatasi na kiwafungia ndani ya kifaa maalum. Wakifanya mapenzi, hukwama mpaka tunawatenganisha,” alisema mganga huyo.