Rais Pombe Magufuli amteua Dkt. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Novemba, 2017 amemteua Dkt. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi.
Dkt. Wilbrod Peter Slaa ataapishwa baada ya taratibu kukamilika. Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam 23 Novemba, 2017