HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 28 Aprili 2018

Jamani jiandaeni kisaikolojia kabisaa!

mwanaspoti.co.tz

FURAHA ya mashabiki wa soka ni ushindi tu na ikitokea mambo tofauti ndio unaona wengine wanazimia uwanjani na kutolewa kwa machela. Kesho ndio ule mtanange wa watani wa jadi, Simba na Yanga ambao kwa kuangalia walivyocheza mechi zao za mwisho na matokeo waliyoyapata basi ni bora unakajiandaa kisaikolojia tu.

Wale wazee wa mkeka wanadai kuwa goma linaweza kumalizika kwa sare ndani ya dakika 90 kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Simba ikijiandaa kucheza na Yanga, mechi yake ya mwisho alicheza na Njombe Mji na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Wapinzani wao Yanga, wakajibu mapigo kwa kuifunga Stand United ya Shinyanga kwa mabao 4-0, matokeo hayo yakazaa sare ya bao 1-1 walipokuja kukutana wenyewe pale Taifa.

Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake, Obrey Chirwa, mashabiki wa Simba wakakosa raha kwa dakika kadha kabla ya winga anayetumia miguu miwili kuuchezea mpira, Shiza Kichuya kuwanyanyua kwenye viti baada ya kusawazisha.

Simba na Yanga, zikijiandaa kucheza mechi ya mzunguko wa pili kesho Jumapili, mechi zao za mwisho zimeambulia pointi moja moja.

Wekundu wa Msimbazi walibanwa mbavu dhidi ya Lipuli pale Uwanja wa Samora mjini Iringa wakati Yanga wakivurugwa na bao la jioni kabisa na Mbeya City.

Kwa kuangalia matokeo hayo, baadhi ya mashabiki wanaamini kuwa goma hilo linaweza kulala tena kwa sare licha ya timu zote kukamiana kwelikweli.

Dalali arusha dongo Jangwani

Yanga imemleta kocha mpya Mkongo, Mwinyi Zahera kubeba mikoba ya Mzambia, George Lwandamina, lakini huko Simba povu linawatoka unaambiwa.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa timu hiyo, Hassani Dalali alisema Yanga wamejitathimini na kuangalia ubora wa wapinzani wao na kuamua kumleta atakayeamua mchezo huo.

“Hii inaonyesha namna Yanga wanavyoiogopa Simba, wamekwenda kucheza mechi ya kimataifa kule Ethiopia wakiwa na kocha msaidizi (Noel Mwandila na Shadrack Nsajigwa) lakini kwa Simba wameona watafute kocha fasta tu,” alisema.

Emmanuel Gabriel aliyetumika ndani ya kikosi cha Simba kama straika, alisema ujio wa Mkongomani huyo unalenga kuiongezea nguvu Yanga.

“Soka lina mbinu nyingi, wapo wachezaji ambao wakikosekana katika mechi hiyo, inatia shaka na ndio kilichotokea kwa Yanga, wameona ni lazima benchi lao likamilike kwanza,” alisema.

Mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Zamoyoni Mogella alisema mechi ya watani imebeba maumivu tofauti na wanapokutana hivyo, walichokifanya Yanga ni kutambua umuhimu wa mchezo huo.

Alisema kutokana na hali ilivyo sasa, kila upande unavutia kwake lakini kikubwa ni kusubiri dakika 90.