Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka kesho Jumapili, April 15 kwenda nchini Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema msafara huo unaondoka kesho utakuwa na wachezaji 20 na viongozi 13 ambapo wanane kati yao ni wa benchi la Ufundi.
Yanga itaikabili Dicha Jumatano ijayo katika mchezo utakaopigwa mji wa Hawassa.
Tayari Yanga iko mbele kwa mabao 2-0 hivyo inahitaji ushindi au matokeo ya sare ili kujihakikishia inasonga mbele hatua ya makundiKikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka kesho Jumapili, April 15 kwenda nchini Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema msafara huo unaondoka kesho utakuwa na wachezaji 20 na viongozi 13 ambapo wanane kati yao ni wa benchi la Ufundi.
Yanga itaikabili Dicha Jumatano ijayo katika mchezo utakaopigwa mji wa Hawassa.
Tayari Yanga iko mbele kwa mabao 2-0 hivyo inahitaji ushindi au matokeo ya sare ili kujihakikishia inasonga mbele hatua ya makundi