HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 24 Aprili 2018

Mbeya city uzembe huu utawagharimu


Mbeya city itabidi ijilaumu yenyewe kwa uzembe wa kumruhusu mchezaji wake kufanya ujanja na kuingia uwanjani bila ruhusa ya muamuzi na wakifahamu kua ni kosa kwa mujibu wa sheria za mpira wa miguu kwa kitendo hicho. Ukiangalia video kuanzia sekunde ya 31 utaona wachezaji wa mbeya city wakiwa kumi uwanjani na ikiwa mmoja tayari amepewa kadi nyekundu. Na kwa mujibu wa sheria 3 ya FIFA kipengele cha tatu utaratibu wa kubadilisha mchezajikosa hilo linaelekezwa kwa mchezaji na sio muamuzi kama wengi wanavyolaumu kwani ni mujibu wa mchezaji kuingia uwanjani pale mchezaji anayebadilishwa naye akiwa nje ya mchezo na sio vinginevyo. Kwa mantiki hiyo benchi la ufundi la mbeay city hawawezi kukwepa adhabu hiyo. nimeambatanisha sehemu ya sheria namba 3 kuhusiana na utaratibu wa kufanya mabadiliko kwenye mchezo wa mpira wa miguu