HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 8 Aprili 2018

Mtambue mwanamke wa kwanza kupata Degree Tanzania


Mtambue mwanamke wa kwanza kupata Degree Tanzania

Dkt. Maria Kamm ndiye  mwanamke wa kwanza wa Tanzania kupata Shahada ya kwanza (Degree) na leo ametunukiwa tuzo ya heshima katika tuzo za Malkia wa Nguvu zinazoandaliwa na Clouds Media.

Mama Kamm ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Weruweru iliyopo Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, akiwa kama Mzalendo wa kweli, ametumia maisha yake kwa kiasi kikubwa kuwashauri na kuwaelimisha vijana katika masuala mbalimbali ya Taifa.

Mgeni Rasmi katika utoaji wa Tuzo hizo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwl Nyerere Posta jijini Dar, alikuwa  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, dkt. ummy Ally Mwalimu.