HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 8 Aprili 2018

Samatta Alazimisha Penati Genk ikishinda Bao moja

Mchezaji Mbwana Samatta usiku wa kuamkia leo ameisaidia klabu yake ya KRC Genk kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Standard Liege, baada ya jitihada zake za kutaka kufunga, kuzaa penalti kufuatia kuangushwa kwenye eneo la 18.

Penalti hiyo ilipatikana baada ya Samatta kuangushwa chini na beki wa Standard Liege, Sebastien Pocognoli wakati akiweka vizuri mpira kwaajili ya kumalizia krosi ya kiungo wa Genk Ruslan Malinovskyi. 

Hata hivyo Samatta hakupiga yeye mkwaju huo badala yake alifanya hivyo mshambuliaji Leandro Trossard mwenye umri wa miaka 23 katika dakika ya 49. Bao hilo lilidumu hadi mpira unamalizika.

Samatta sasa anaonekana kuimalika baada ya kucheza dakika zote 90 ikiwa ni mara yake ya pili tangu apone maumivu ya goti yaliyomweka nje kwa muda mrefu. Pia mechi ya jana ilikuwa ni ya 81 tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe.