Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar, Lazaro Mambosasa amesema kuwa, mpaka sasa watu tisa wameripotiwa kufariki kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, huku wengine 6 wakijeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta.
Amesema baadhi ya waliofariki miili yao ilikutwa ikielea.