HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 15 Aprili 2018

Zari Amtukana Diamond Kwa Kushindwa Kuwajali Watoto

Zari Amtukana Diamond Kwa Kushindwa Kuwajali Watoto

Aliyekuwa mpenzi wa Diamond Platinumz ambaye ni mama wa watoto wawili wa msanii huyo, Zari The Boss Lady ameshindwa kuficha hasira zake na kumshambulia kwa matusi mtandaoni.

Mashambulizi ya Zari aliyoyatoa kupitia snapchat, muda mfupi kabla hajaelekea kanisani yalionekana yakihusishwa na ujumbe ambao Diamond aliuandika kwenye Instagram kuhusu wanawake akipigia debe tukio linalofywa leo na Zamaradi Mketema.

“Ikiwa Mama yangu alinilea Pekee hadi kufika hapa…Naamini Mwanamke ni Kiongozi bora Mwenye kuweza kuleta Maendeleo na Furaha ya Kweli Ulimwenguni….Please Tag wanake wote Wapambanaji na Wapenda Maendeleo waambie @zamaradimketemaKawaandalia jambo Kesho [leo],” aliandika Diamond.

Dakika chache baadaye, Zari aliweka ujumbe wake uliojaa hasira akitumia maneno makali na kumuita Diamond ‘mjinga’. Ingawa hakumtaja jina, kitendo cha kumkosoa kwa kushindwa kuwaona watoto wake kwa muda mrefu kinaonesha kuwa anayezungumziwa ni baba Tifah.
Baadaye, Zari aliweka picha inayomuonesha akiwa mbele ya kioo na nguo nyingi na kuandika ujumbe kuwa ni muda wa kanisani.