HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 5 Mei 2018

Yondani, Tshishimbi waichanganya Yanga

MAMBO yanaonekana kutokuwa sawa ndani ya klabu ya Yanga baada ya nyota wake wakiongozwa na Kelvin Yondani na Papy Tshishimbi kutoungana na wenzano kwenye safari ya Algeria.

Yanga ipo nchini humo ikijiandaa kucheza mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaochezwa kesho usiku.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa zinasema kuna mgomo baridi kutoka kwa baadhi ya nyota wake.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya timu hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa viongozi wanajaribu kuficha mambo lakini ukweli kuna mvutano ndani ya kikosi hicho.

“Haiwezekani wachezaji wanatoweka na kuzima simu wakati tunakabiriwa na mchezo muhimu, wamegoma na ndio maana hawajaondoka,” alisema Mjumbe.

“Hakuna anayeumwa, Ajibu (Ibrahimu), Yondani, Tshishimbi na hata Chirwa wote wazima ila kuna mgomo,” alisema.

Alipoulizwa na gazeti hili juu ya suala la wachezaji hao ‘walioingia mitini’, Afisa habari wa Yanga, Dismas Ten, alikataa kuzungumza lolote na kumtaka mwandishi kumtafuta baada ya saa moja.

“Nipo Azam Media ngoja nikirudi ofisini nitakuwa na kitu cha kuongea kwa sasa siwezi ila ni kweli wachezaji hao hawajasafiri.., nitafute baada ya saa moja,” alisema Ten.

Hata hivyo alipotafutwa tena baadae simu yake ya mkononi ilikuwa imezimwa.

Nyota ambao hawajasafiri na timu hiyo bila sababu za kuelekeweka ni Ibrahim Ajibu, Yondani, Chirwa na Tshishimbi.